Location: Dar Es Salaam
Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke anawatangazia Wananchi/ Watanzania wote wenye sifa zinazotakiwa kuomba kujaza nafasi mbalimbali za kazi kama zilivyoainishwa hapo chini:-
NAFASI ZA KAZI
Katibu Mahsusi Daraja La III (Nafasi 2)
SIFA/ELIMU/UJUZI
• Elimu ya kidato cha IV.
• Waliohudhuria mafunzo ya uhaziJ! na kufaulu mtihani wa hatua ya III.
• Waliofaulu s,omo la hati mkato ya Kiswahili na kiingereza maneno 80 kwa dakika 1.
• Waliopata mafunzo ya Kompyuta kutoka katika Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali na kupata cheti katika programme ya windows/Microsoft Office/ Internet/Email na Publisher.
KAZI NA MAJUKUMU
• Kuchapa barua/taarifa na nyaraka za kawaida.
• Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao na kuwaelekeza sehemu wanaweza kushunghulikiwa.
• Kusaidia kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za mkuu wake, na ratiba za kazi zingine zilizotangwa kutekelezwa katika ofisi anamofanyia kazi na kumwa’rifu mkuu wake kwa wakati unapohitajika.
• Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake majalada, nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika shunghuli za kazi hapo Ofisini.
• Kusaidia kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake na pia kumwarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao.
• Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa Maofisa walio katika sehemu alipo, na kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu inayohusika.
• Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na msaidizi wake wa kazi.
NGAZI VA MSHAHARA
• Ataanza mshahara TGS B (1) kwa mujibu wa viwango vya Serikalini.
UMRI
Waombaji wote wanatakiwa wawe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 45.
MAELEZO YA JUMLA
Maombi yote yawasilishwe yakiwa yameambatanishiwa na CV pamoja na nakala za vyeti vya kuhitimu elimu na mafunzo (vyeti vinavyoonyesha kiwango cha kufaulu na sio ‘leaving certificate’)
MUHIMU
Muombaji anatakiwa atume vyeti vyake halisi na halali kwani uhakiki utafanyika katika vyuo alivyopitia parnoja na Baraza la Mitihani. Udanganyifu wowote ukibainika hatua za kisheria zitachukuliwa.
MAOMBI VATUMWE KWA ANWANI IFUATAVO:-
MKURUGENZI WA MANISPAA
HALMASHAURI VA MANISPAA VA TEMEKE
S.L.P 46343, DAR ES SALAAM
Application deadline 2017-08-25